Kisii University Institutional Repository

Uchanganuzi wa Lugha ya Kisitiari Katika Kusawiri Siasa Katika Riwaya ya Kiswahili: Mfano wa Chozi la Heri Na Kiza Katika Nuru

Show simple item record

dc.contributor.author Mumo, King’oo Faith
dc.date.accessioned 2025-11-14T09:08:23Z
dc.date.available 2025-11-14T09:08:23Z
dc.date.issued 2025-10
dc.identifier.other MAS16/60247/15
dc.identifier.uri http://localhost:8080/xmlui/handle/123456789/10114
dc.description.abstract Katika uwasilishaji wa kazi yoyote ya kifasihi, lugha huwa kipengele cha umuhimu sana. Utafiti huu ulinuia kuchunguza lugha ya kisitiari katika usawiri wa masuala ya kisiasa katika riwaya ya Kiza katika Nuru na Chozi la Heri. Utafiti ulizingatia malengo yafuatayo: Kudhihirisha matumizi ya lugha ya kisitiari ili kusawiri siasa katika Chozi la Heri na Kiza katika Nuru, Kufafanua taashira zilizojengwa na lugha ya kisitiari katika Chozi la Heri na Kiza katika Nuru, Kutathmini jinsi lugha ya kisitiari ilivyotumika katika kuwaumba wahusika ili kuibua masuala ya kisiasa katika Kiza katika Nuru na Chozi la Heri. Utafiti uliongozwa na nadharia ya umitindo iliyoasisiwa na Viktor Shklovsky mwaka wa 1904. Kulingana na nadharia hii, mwandishi wa kazi za kifasihi hutumia lugha yenye maana fiche huku akimuwezesha msomaji kuwa na mwelekeo mpya kuhusu kitu cha kawaida tu. Mhimili mkuu wa nadharia ya umitindo ni kwamba maana katika kazi za fasihi huwasilishwa kwa njia fiche. Mwandishi wa kazi za fasihi hutumia lugha ya kitamathali kama vile tashbihi, taashira, methali, misemo miongoni mwa zingine ili kupata mtindo usio wa moja kwa moja. Utafiti ulichukua muundo elezi. Katika usampulishaji, riwaya zilizoteuliwa ni pamoja na Chozi la Heri na Kiza katika Nuru. Riwaya hizi ziliteuliwa kimaksudi kwa sababu baada ya usomaji wa awali ilidhihirika kwamba lugha ya kisitiari katika kuibua masuala ya kisiasa imejitokeza mno. Ukusanyaji wa data ulijumuisha kusoma riwaya teule na kudondoa vipengele vya lugha ya kisitiari vilivyobeba masuala ya kisiasa. Aidha, kazi zingine zilizokuwa na umuhimu katika utafiti huu zilirejelewa. Baada ya kukusanya data, uchanganuzi na uhariri wa data hiyo uliendelezwa huku ukiongozwa na nadharia na malengo ya utafiti. Utafiti ulibaini kuwa waandishi wa riwaya ya Kiza katika Nuru na Chozi la Heri wametumia lugha ya kisitiari sana kujenga masuala ya kisiasa. Waandishi wa riwaya hizi wamefanikisha kazi zao kifani kupitia matumizi ya lugha ya kisitiari katika kujenga masuala ya kisiasa. Masuala ya kisiasa yaliyojengwa na mbinu hizi ni pamoja na: upigaji kura, vita vya baada ya uchaguzi, viongozi kutumia vijana kuendeleza mapigano, ufisadi, nafasi ya mwanamke katika siasa/uongozi, dhuluma kwa raia, kuuliwa kwa wapinzani na watetezi wa haki miongoni mwa mengine. Kitaalamu, matokeo ya utafiti huu yatawanufaisha wasomaji na wahakiki wa riwaya ya Kiswahili katika kuelewa zaidi kuhusu jinsi lugha ya kisitiari imetumika katika kujenga masuala ya kisiasa katika riwaya ya Kiswahili. Kinadharia, utafiti huu utawafaa watafiti wengine watakaotumia nadharia ya umitindo katika kuchanganua kazi zingine za kifasihi. Inapendekezwa kwamba watafiti wengine wanaweza kuchuguza matumizi ya lugha ya kisitiari katika kuibua masuala mengine yasiyo ya kisiasa katika riwaya ya Kiswahili. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.publisher Kisii University en_US
dc.subject Uchanganuzi wa Lugha ya Kisitiari en_US
dc.subject Kusawiri Siasa Katika Riwaya ya Kiswahili en_US
dc.subject Chozi la Heri en_US
dc.subject Kiza Katika Nuru en_US
dc.title Uchanganuzi wa Lugha ya Kisitiari Katika Kusawiri Siasa Katika Riwaya ya Kiswahili: Mfano wa Chozi la Heri Na Kiza Katika Nuru en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Advanced Search

Browse

My Account